WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Monday, November 5, 2012

YANGA YAKAMATA UONGOZI WA LIGI

Hatimaye, baada ya harakati na mbio za kupanda katika msimamo wa Ligi, Timu ya Yanga imefanikiwa kufika kileleni mwa ligi ya Vodacom na kuwapiku watani wake wa jadi Simba. Uongozi wa ligi hii unatokana na timu ya Yanga kuifunga timu ya Azam mabao 2 - 0 kwenye uwanja wa taifa huku waliokuwa viongozi wa Ligi, Simba wakifungwa 2 - 0 na timu ya Mtibwa huko Morogoro.
 Ushindi huu wa Yanga ambao umepeleka furaha Jangwani ulifanikishwa kwa Magoli yaliyofungwa na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza na kuifanya Yanga ifikishe Jumla ya Pointi 25.
Kikosi cha Yanga kilichopeleka kilio Azam
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ulishuhudiwa Kuvunjwa kwa Rekodi ya Timu ya Simba ya Kutofungwa tangu kuanza kwa Ligi. Rekodi hiyo ilivunjwa kwa msaada wa washambuliaji Mohamed Mkopi na Hussein javu wa timu ya Mtibwa.

 

No comments:

Post a Comment