WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Thursday, October 11, 2012

YANGA YAPATA USHINDI DHIDI YA TOTO AFRICA

Wachezaji wa Yanga wakishangilia Ushindi - Uwanja wa Kirumba Mwanza
Yanga ilishinda katika Mchezo huo kwa Magoli 3 - 1
Magoli mawili ya Kipindi Cha kwanza ya Yanga Dakika ya Pili la Didier Kavumbagu na Mbyu Twite lilopatikana Dakika ya 21 yalifanya Timu ya Jangwani iende Mapumziko ikiwa Kifua Mbele kwa magoli Mawili. Kipindi Cha pili kilipoanza kilishuhudia Mchezaji Jerry Tegete akifumania nyavu za Toto Afican katika Dakika ya 69 na kuhitimisha Mvua ya Magoli kutoka kwa vijana hawa Jangwani. Goli la Said Mussa wa Toto Africa ndilo lilipeleka kifuta Machozi kwa Vijana hawa wa Mwanza ambao walivunja rekodi ya kuifunga timu hii ya Jangani katika Msimu uliopita

Matokeo haya  ni Faraja kwa timu hii lakini hasa kwa Kocha Muholanzi Johannes Brandts aliyetokea APR Rwanda kuja kuvaa viatu vyaTom Saintfiet ambaya mkataba wake ulikatishwa kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Matokeo haya yanaifanya Yanga kujiongezea pointi Tatu na kuwa na Pointi 11 kwenye Msimamo wa Ligi
Furaha kwa Wachezaji wa Yanga Baada ya Kuifunga Toto Africa
Yanga ilishinda katika Mchezo huo kwa Magoli 3 - 1

No comments:

Post a Comment