WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Sunday, November 25, 2012

KOCHA MPYA WA CHELSEA AZOMEWA UWANJANI

Rafael Benitez, Kocha mpya wa Chelsea aliyechukua nafasi ya Kocha aliyeondolewa DiMateo alikutana na wakati mgumu jana wakati akikiongoza kikosi hicho cha Stamford Bridge katika Mechi baina ya Chelsea na Manchester City.

Mechi hii ngumu iliyoikutanisha miamba ya soka katita Ligi ya Uingereza, ilifanyika katika uwanja wa nyumbani wa Chelsea, Stamford Bridge. Mara tu Kocha Rafael Benitez alipoingia alikutana na miluzi na kelele za kuzomea "Boooo- booo- booo!" toka kwa baadhi ya mashabiki wa timu ya Chelsea.
Rafael Benitez aliwahi kuwa kocha wa timu ya Liverpool ambayo ni kati ya Mahasimu wakuu wa timu hiyo ya Chelsea.

Kulikuwa na vibao mbalimbali vilivyoonekana kumuenzi Kocha aliyekatishiwa mkataba DiMateo na kumponda Rafael kama Vile "There's only one Di Matteo", "Rafa Out", "DiMateo CFC Legend Thank you", "Only one DiMateo" In Roberto we Trusted and Loved In Rafa We Will Never Trust! Fact!"







Kutokana na Matukio hayo, Golikipa wa Chelsea Petr Cech amewaomba mashabiki wa Chelsea wampe Benitez Muda baada ya yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na kuzomewa na kutoka sare katika mechi hiyo ambayo ni ya kwanza tangu aliposaini mkataba wa kuifundisha Chelsea.

No comments:

Post a Comment