WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Friday, November 23, 2012

SANAMU YA SIR ALEX FERGUSON YAZINDULIWA

Sanamu iliyojengwa kwa Heshima ya Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, ambaye ameitumikia timu kwa Miaka 26, tangu Tarehe 6 Novemba 1986 imezinduliwa Rasmi leo tarehe 23 Novemba 2012 Old Trafford.
Uzinduzi huu ulihudhuriwa na wachezaji wote wa kikosi cha Kwanza cha Manchester United, Wachezaji maarufu wa zamani kama Eric Cantona, Ruud van Nistelrooy, Ole Gunnar Solskjaer, Dwight Yorke, Andy Cole, Edwin vander Sar, Peter Schmeichel, Gary na Phill Nevile.

David Beckam na Cristian Ronaldo hawakuweza kuhudhuria lakini walituma ujumbe wa Sauti kumpongeza Kocha wao kama ambavyo alifanya Raisi wa Fifa Sepp Blatter ambaye hakuweza kuhudhuria.
Sir Alex Ferguson alionyesha furaha yake kwa kusema kuwa anajivunia uzinduzi huo kwa vile watu hufa bila kuziona Sanamu zao lakini yeye ni kama mfu aliyefufuka na kuiona sanamu yake. Aliwashukuru wachezaji wote baadhi yao wakiwa wamehudhuria uzinduzi huo kwa vile wameleta furaha siku zote katika klabu ya manchester United.

 
Sanamu ya Futi Tisa ya Alex Ferguson, Old Trafford
 
 
Sanamu ya Alex Ferguson, ikifunuliwa kwa uzinduzi
Mfungaji wa Zamani Eric Cantona na Van Nistelrooy wakati wa Uzinduzi
Mfungaji Machachari wa Manchester United Dwight Yorke alihudhuria uzinduzi pia

No comments:

Post a Comment