WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Tuesday, July 31, 2012

YANGA YATWAA UBINGWA KOMBE LA KAGAME


Hatimaye timu ya Young Africans( Yanga ) ya Dar es Salaam imefanikiwa kutetea ubingwa wake na kutwaa kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga timu ya Azam FC Kwa magoli  2-1. Hata hivyo kwa Timu ya Azam FC hatua hiyo iliyofika ni ya kujivunia kwa vile ni kwa Mara ya Kwanza inashiriki katika Mashindano haya na kufanikiwa kufika hatua ya Fainali.
Mchezo ulianza kwa vijana wa Azam kuonyesha utulivu na umiliki wa mpira ukilinganisha na Yanga ambao hawakuanza vizuri mchezo. Bao la Hamis Kiiza katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza liliamsha ari , nderemo na vifijo kwa mashabiki na wachezaji wa klabu hiyo kongwe na maarufu ya mtaa wa Jangwani.

Yanga walijipanga vizuri na kupeleka mashambulizi makali kwa wapinzani wao Azam FC katika kipindi cha pili cha mchezo huku Azam nao wakifanya kila waliloweza kukabiliana na ari hiyo ya kulibakiza Kombe la Kagame pale Jangwani. Kasi hii ya Yanga ilizaa matunda katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza katika kipindi cha pili ambapo mchezaji aliyekuwa tishio katika Ngome ya Azam, Said Bahanuzi alipoipatia Yanga goli la pili lililopiga msumari wa Mwisho na kuihakikishia Yanga Ushindi.

Kipenga cha mwisho katika mpambano huu kilihitimisha mbio za kinyang'anyiro cha mashindano ya Kagame mwaka 2012 na kuitawaza rasmi kalbuya  yanga kuwa kuwa mshindi wa kombe la Kagame na kufikisha rekodi ya mara tano ya kutwaa kombe hilo ambapo walitwaa kombe hilo mwaka 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.

Ushindi huu umetoa salamu tosha toka kwa Uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa hivi karibuni, Kocha mpya wa Yanga aliyesaini kuifundisha klabu hiyo ya Jangwani msimu huu na kuonyesha Makucha ya kikosi kipya cha Yanga 2012/13.

Tunaipongeza klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Kagame kwa Mara nyingine tena.

No comments:

Post a Comment