WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Thursday, June 7, 2012

BURUDANI INAANZA EURO 2012 LEO



Ule wakati uliokuwa unangojewa kwa hamu hatimaye umewadia ambapo kinyang’anyiro cha kombe la mataifa ya Ulaya 2012 kitaanza huko Poland na Ukraine, nchi ambazo ni wenyeji wa mashindano hayo ya Ulaya mwaka huu. Mashindano haya ya Ulaya (UEFA European Football Championship) yajulikanayo kama EURO 2012 ni ya kumi na nne (14) kuandaliwa na UEFA. Mashindano haya yanaanza rasmi leo Ijumaa tarehe 8 Juni na yanatarajiwa kumalizika tarehe 1 Julai 2012 mjini Kiev.

Mashindano haya yanashirikisha timu bora 16 kutoka mataifa ya Ulaya zitakazoumana katika michezo 31 ndani ya wiki tatu katika viwanja Nane vya Poland na Ukraine. Viwanja vitakavyoumika na uwezo wake kwenye mabano ni Warsaw (58,500), Gdansk (43,600), Wroclaw (42,800), Poznan (43,300), Kiev (60,00), Lviv (30,000), Donetsk (50,000) na Kharkiv (35,000). Ukiachia viwanja vya Poznan na Kharkiv ambavyo vimefanyiwa matengenezo makubwa, viwanja sita vilivyobaki ni vipya kabisa.

Michezo itakayochezwa kwenye viwanja hivi ni
KIWANJA
MECHI
ROBO FAINAL
NUSU FAINALI
FAINALI
Warsaw
Mechi 3 Kundi A
1
1

Gdansk
Mechi 3 Kundi C
1


Wroclaw
Mechi 3 Kundi A



Poznan
Mechi 3 Kundi C



Kiev
Mechi 3 Kundi D
1

1
Lviv
Mechi 3 Kundi B



Donetsk
Mechi 3 Kundi D
1
1

Kharkiv
Mechi 3 Kundi B




Kutakuwa na Makundi manne katika mashindano haya kama ilivyoanishwa hapa chini:
KUNDI A
KUNDI B
KUNDI C
KUNDI D
Poland
Netherlands
Spain
Ukraine
Greece
Denmark
Italy
Sweden
Russia
Germany
Republic of Ireland
France
Czech Republic
Portugal
Croatia
England


RATIBA YA MASHINDANO YA EURO 2012
SIKU
KUNDI
MECHI
Ijumaa 8 Juni 2012
A
Poland V Greece
A
Russia V Czech Rep
Jumamosi 9 Juni 2012
B
Netherlands V Denmark
B
German V Portugal
Jumapili 10 Juni 2012
C
Spain V Italy
C
Ireland V Croatia
Jumatatu 11 Juni 2012
D
France V England
D
Ukraine V Sweden
Jumanne 12 2012
A
Greece v Czech
A
Poland V Russia
Jumatano 13 Juni 2012
B
Denmark V Portugal
B
Netherlands V Germany
Alhamisi 14 Juni 2012
C
Italy V Croatia
C
Spain V Ireland
Ijumaa 15 Juni 2012
D
Ukraine V France
D
Sweden V England
Jumamosi 16 Juni 2012
A
Czech V Poland
A
Greece V Russia
Jumapili 17 Juni 2012
B
Denmark V Germany
B
Portugal V Netherlands
Jumatatu 18 Juni 2012
C
Croatia V Spain
C
Italy V Ireland
Jumanne 19 Juni 2012
D
England V Ukraine
D
Sweden V France
EURO 2012 KARIBUNI POLAND! KARIBUNI UKRAINE!



No comments:

Post a Comment