WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Monday, May 28, 2012

Golikipa aiyeiokoa Chelsea Petr Cech (30) Asaini Mkataba wa Miaka 4


Petr aliyeokoa michomo mitatu ya penati toka kwa Bayrn Munich na kufanikisha kuipa ubingwa wa Kombe la Ulaya timu yake ya Chelsea, amesaini mkataba wa miaka mine na Chelsea.

Petr Cech alijiunga na Chelsea mwaka 2004 ambako amecheza Mechi 369, ikiwa ni mechi nyingi zaidi kuchezwa na mchezaji  kutoka nje ya Uingereza katika klabu hiyo. 

Mechi hizo zimeshuhudia chesea ikishinda vikombe katika mashindano manne tofauti yaani Ligi ya Uingereza (EPL) mara tatu, Kombe la FA mara mara nne, Kombe la Carling mara mbili na Kombe la mabingwa wa Ulaya mara moja.

Baada ya kusaini mkataba Cech alisema anafuraha kubwa kuwa sehemu ya timu kubwa ya Chelsea kwa miaka mingine minne huku akiamini kuwa miaka hiyo minned itakuwa ya mafanikio kama ilvyokuwa miaka nane iliyopita.

Petr Cech ametoa mchango mkubwa sana katika ushindi wa timu yake ya Chelsea kwenye Kombe la FA na lile la mabingwa wa ulaya kwa kuokoa mikwaju mbalimbali golini kwake ambayo ingesababusha madhara.
Atakubukwa pia kwa kuokoa mkwaju wa penati wa Arjen Robben wa Bayern Munich katika fainali ya Kombe la mabingea katika muda wa nyongeza na kuokoa peati mbili pia wakati wa kipindi cha kupigiana mikwaju ya penati baada ya kumalizika kwa muda wa nyongeza huku timu hizi zikiwa sare.

Mkurugenzi wa timu ya Chelsea Ron Gourlay alisema kuwa anathamini mchango mkubwa wa Petr Cech kaika kipindi hikik cha mafanikio makubwa kwa Chelsea na wamefurahi kuwa naye tena katika kipindi hiki mpaka mwaka 2016.


No comments:

Post a Comment