Baada
ya Shauku, hamasa na kukamiana, hatimaye Goli la Vincent Kompany liliamua
Mshindi wa Manchester Derby. Ushindi huu umewapaisha Manchester City kileleni
mwa msimamo wa ligi baada ya kutwaa kwa mara nyingine usukunani wa ligi. Goli
hili lililofungwa mwishoni mwa kipindi cha pili kwa kuunganisha mpira wa kona lilidumu
mpaka mwisho wa mchezo.
Kompany akiunganisha mkwaju wa Kona kimiani
Kompany akifurahia goli lake la kwa shangwe
Hebu
tujikumbushe Goli hilo lilivyofungwa….
Matokeo haya
yanazidi kufanya kinyang’anyiro cha ubingwa wa kombe la ligi ya Uingereza kuwa
gumu sana huku ukiipa nafasi kubwa Manchester City endapo timu zote mbili
(Manchester city na Manchester United) zitashinda katika mechi zilizobaki.
Matokeo haya yanazifanya
timu hizi mbili kufungana kwa pointi na kutofautiana kwa idadi kubwa ya Magoli
ambayo yanaiweka Manchester City katika Nafasi nzuri zaidi.
Manchester City
inataka kutwaa ubingwa wa mashindano haya kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya
hivyo mwaka 1968 huku wakiwa na mechi ngumu mbele yao dhidi ya New Castle
United.
No comments:
Post a Comment