WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Monday, May 14, 2012

Manchester City Ndio Mabingwa wa EPL


Picha kwa Hisani ya Alex Livesey/Getty Images)


Baada ya Dakika 90 zilizokuwa ngumu zaidi kwa watazamaji na Mashabiki wa timu mbalimbali zinazo shiriki Ligi ya Uingereza EPL hatimaye mshindi alipatikana. Michezo kumi ilikuwa ikiendelea katika viwanja mbalimbali vya Uingereza katika kukamilisha mizunguko 38 ya ligi ya uingereza..Wasiwasi mkubwa ulikuwa kwa timu zinazowania ubingwa yaani Manchester United na mancester City, Timu tatu yaani Arsenal, Tottenham and Newcastle  zilikuwa zikipigana vikumbo kugombea kuwemo katika ligi ya Mabingwa (Champions League) Huku QPR na Bolton  zikipigana kuepuka kushuka Daraja.


Dakika 90 katika Uwanja wa Etihad ambako mchezo ulitawaliwa na matukio ya kushtusha, kushangaza na kuleta shinikizo la hisia ambapo QPR ilishangaza mashabiki na watizamaji pale iliposhika usukani wa mchezo kwa kipindi kirefu huku ikiwa na wachezaji pungufu. 

Pigo kwa QPR wakati Joey Barton aliooneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga Tevez kwa kiwiko "Kisukusuku ama Ki-pepsi"

Sergio Aguero akihitimisha kitendawili cha Ubingwa wa ligi ya Uingereza

Hatimaye goli la dakika ya 93 la Sergio Aguero likaondoa hofu kwa Manchester City na kupeleka kilio kwa QPR na kuifanya Manchester City kuwa Bingwa wa Ligi ya Uingereza baada ya Miaka 44 kwa ushindi wa magoli 3 – 2.

Goli la Sergio Aguero...


Matokeo ya Mwishoni mwa wiki yaliyohitimisha ligi ya Uingereza ni kama yanavyoonekana hapa chini.

Mechi
Timu
Mshindi
1
Chelsea 2-1 Blackburn
Chelsea
2
Everton 3-1 Newcastle
Everton
3
Man City 3-2 QPR
Manchester City
4
Norwich 2-0 Aston Villa
Norwich
5
Stoke 2-2 Bolton
Sare
6
Sunderland 0-1 Manchester United
Manchester United
7
Swansea 1-0 Liverpool
Swansea
8
Tottenham 2-0 Fulham
Tottenham
9
West Brom 2-3 Arsenal
Arsenal
10
Wigan 3-2 Wolves
Wigan


Ligi ya Uingereza inamalizika huku miamba miwili ikifungana kwa pointi na kutofautiana katika magoli ya kufunga. Ulikuwa mwisho wa ligi machachari, wenye hamasa utakaokumbukwa kutokana na timu nyingi kupata mashabiki wa mkopo kwani ushindi au kushindwa kwa timu Fulani kulikuwa na athari kwa timu nyingine ama katika kupata nafasi nne za juu ama kushuka daraja.



Ligi ya Uingereza imemalizika ikiwa na Msimamo huu:

Team
P
Home W
D
L
F
A
Away W
D
L
F
A
GD
Pts
Man City
38
18
1
0
55
12
10
4
5
38
17
64
89
Man United
38
15
2
2
52
19
13
3
3
37
14
56
89
Arsenal
38
12
4
3
39
17
9
3
7
35
32
25
70
Tottenham
38
13
3
3
39
17
7
6
6
27
24
25
69
Newcastle
38
11
5
3
29
17
8
3
8
27
34
5
65
Chelsea
38
12
3
4
41
24
6
7
6
24
22
19
64
Everton
38
10
3
6
28
15
5
8
6
22
25
10
56
Liverpool
38
6
9
4
24
16
8
1
10
23
24
7
52
Fulham
38
10
5
4
36
26
4
5
10
12
25
-3
52
West Brom
38
6
3
10
21
22
7
5
7
24
30
-7
47
Swansea
38
8
7
4
27
18
4
4
11
17
33
-7
47
Norwich
38
7
6
6
28
30
5
5
9
24
36
-14
47
Sunderland
38
7
7
5
26
17
4
5
10
19
29
-1
45
Stoke
38
7
8
4
25
20
4
4
11
11
33
-17
45
Wigan
38
5
7
7
22
27
6
3
10
20
35
-20
43
Aston Villa
38
4
7
8
20
25
3
10
6
17
28
-16
38
QPR
38
7
5
7
24
25
3
2
14
19
41
-23
37
Bolton
38
4
4
11
23
39
6
2
11
23
38
-31
36
Blackburn
38
6
1
12
26
33
2
6
11
22
45
-30
31
Wolves
38
3
3
13
19
43
2
7
10
21
39
-42
25


Furaha ya kuchukua ubingwa baada ya Miongo minne (yaani miaka 44)....

Hongera, Manchester City kwa Ushindi na kuchukua kombe la Ubingwa wa Ligi ya Uingereza (EPL)

No comments:

Post a Comment