Patrick Mafisango
Tumepokea habari kutoka Radio One kuwa kiungo wa Simba, Patrick Mafisango (25) amefariki kwa ajali ya Gari, Tazara Dar es Salaam Leo asubuhi. Mafisango alikuwa akirejea nyumbani akitokea kwenye burudani ya Muziki.
Patrick Mutesa Mafisango ambaye ni
Raia wa Rwanda,alikuwa akichezea timu ya Azm kabla hajajiunga na timu ya
wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club. Patrick mafisango aliwahi kuzichezea timu
kama Atraco na APR za Rwanda Huku akiwa kiungo katika timu ya Taifa ya Rwanda, Amavubi.
Patrick Mafisango akiwa Azam FC ya Dar es Salaam
Akiwa Azam FC
Mafisango wakati akiwa na imu ya Jeshi APR ya Rwanda
Kapteni wa Timu ya APR Patrick Mafisango akiwa ameshikilia kombe la Cecafa Kagame Cup 2010 baada ya kuifunga St. George
Umaarufu wa Mchezaji huyo Kiungo
ulizidi kuongezeka akiwa na Timu ya Simba hasa katika msimu huu ambapo
upachikaji wake wa magoli na Pasi zilizozaa magoli.
Mwenyezi Mungu aliaze Roho ya Marehemu Patrick Mafisango Peponi
No comments:
Post a Comment