(Picha kwa hisani ya Andrew Snell wa Gazeti la SUN Uingereza na Wikipedia)
Rihana (24) alitokezea kwenye Red Carpet katika Onyesho la kwanza la
Sinema ya Battleship akiwa na nguo yake Nyeupe yenye Mgongo wazi huku
ikionyesha tattoo yake siku chache baada ya kutoka Hospitali alikokuwa
amelazwa.
Rihana akiwa katika Muondoko La Premiere Battleship!
Sinema ya Battleship ni sinema ya kivita inayohusisha vionjo vya
kisanyansi ya Kimarekani ya Mwaka 2012. Sinema hii ilipangwa kuzinduliwa mwaka
2011 lakini ikasogezwa mbele mpaka mwezi wa April 2012 kule Uingereza na kisha tarehe
18 mwezi Mei 2012 kule Marekani. Sinema hii pia ipo kwenye mbao za matangazo
pale Mlimani City, Dar es Salaam.
Battleship May 2012
Angalia Trailer ya Sinema ya Battleship ambayo Rihana ameshiriki..
Trailer ya Battleship
Ni kwa mara nyingine Rihana anatokezea kwenye maonyesha makubwa wakati huu
ikiwa ni kwa hisani ya Sinema mpya ambayo ameshiriki ya Battleship. Rihana alionekana Mchangamfu na Mwenye Nguvu tofauti na
ilivyotegemewa baada ya Rihana kutuma picha yake kwenye mtandao wa kijamii wa
Twitter akiwa hospitali ambako alikuwa amelazwa na kuwekewa Drip kutokana na
Uchovu na kupoteza maji mwilini (Dehydration). Kitendo hiki cha kutokezea
kwenye Red Carpet Kilivuta hisia za watu wengi na hasa wapigapicha ambao
walijitahidi kupata picha nzuri ya tukio hili.
Picha ya Mkono wa Rihana uliowekewa Drip, hospitali
Gauni la Rihana Mgongo wazi na Tatoo mguu wa kushoto
Gauni alilolivaa Rihana likimuonyesha akiwa
amesimama upande Tatoo ikionekana
No comments:
Post a Comment