WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Wednesday, May 16, 2012

Kibarua Cha Kenny Daglish Chaota Mbawa...


Mwisho wa Msimu wa ligi huja na msisimko katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ajira, usajilii, mipango na mikakati kwa ajili ya msimu ujao n.k Haya yote hutokana na uzoefu uliopatikana katika msimu uliokwisha. Msisimko huu umemkuta pia Meneja wa Liverpool bwana Kenny Daglish!
Kenny Daglish 
(Picha kwa Hisani ya Gatee Images)

Baada ya miezi 18 akiwa meneja wa kikosi cha Liverpool, Bwana Kenny Daglish, amefungashiwa virago na wenye mali John Henry na Tom Werner mjini Boston ili akatafute Riziki sehemu nyingine, kwani Riziki popote… Wenye mali hawakuridhishwa na matokeo ya Msimu huu ambapo zaidi ya Liverpool kufika fainali ya FA na kuchukua Kombe la Carling, timu hiyo imemaliza ligi kuu ya England ikiwa nafasi ya nane huku ikipoteza michezo mingi na kutokubaliana na sababu zilizokuwa zikitolewa hasa pale iliposhindwa kuqualify kuingia katika Nne Bora ili kujihakikishia ushiriki katika kombe la Mabingwa.

Kufa kufaana kwa ni Majina kama Roberto Martinez Kocha Mkuu wa Wigan na Rafael Benitez Kocha wa zamani wa Liverpool  yameanza kutajwa kuziba nafasi inayoachwa wazi na Kenny Daglish......
Roberto Martinez
Rafael Benitez

Haya ndiyo ni kati ya mengi yatokanayo na Msimu wa ligi 2011/12....

2 comments:

  1. Replies
    1. Mategemeo yalikuwa makubwa sana baada ya KD kuingia Liverpool lakini Matumizi katika usajili na performance ya timu; vilionyesha wazi kuwa kama Livepool inataka kutunza heshima yake basi mabadiliko ilikuwa ni lazima....

      Delete