Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kuikutanisha
miamba miwili ya soka Bayern Munich na Chelsea imewadia. Timu hizi
zilizofanikiwa kuingia katika fainali zitakutana usiku huu pale Fußball Arena
München (Allianz Arena) -Nyasi zitawaka moto!
Timu hizi zimefikia hatua hii baada ya kushinda katika
michezo yao ya fainali ambapo Chelsea ambayo inakaribishwa Mjini Munich
ilikiondoa kigogo cha Soka na klabu bingwa ya dunia, Barcelona ya Hispania huku
Bayern Munich ikiiondoa timu nyingine ngumu ya Hispania Real Madrid.
Jiji la Munich limetawaliwa na homa ya mchezo huu wa
fainali huku mashabiki wa timu zote mbili wakiwa wameifunika mitaa ya Munich
wakiwa wamevalia jezi za timu zao huku wakipeperusha bendera kuzitakiwa ushindi
timu zao.
Homa hii haipo tu kwa mashabiki na wachezaji bali ipo kwa
kiasi kikubwa kwa makocha wa timu hizi; Jupp Heynckes wa Bayern Munich na Roberto Di Matteo wa Chelsea FC
Bayern Munich wanaingia uwanjani leo
wakiwa na historia katika mashindano haya ambapo wamewahi kushiriki fainali
kama hizi na kuchukua ubingwa. Bayern Munich wameshachukua ubingwa wa kombe
hili mara nne (4) na kuwa washindi wa Pili mara nne. Hii ni mara ya tano Bayern
Munich wanakutana na timu ya Chelsea katika ligi ya Mabingwa.
Chelsea walikaribia kunyakuwa ushindi
wa kombe hili pale ilipokutana na timu ya Manchester United na ikakosa ubingwa
huo pale John Terry alipokosa Penati. Chelsea imeshawahi kufikia Nusu fainali
na robo fainali bila kuchukua ubingwa mara nyingi katika ligi ya mabingwa.
Chelsea leo watamkosa John Terry
kutokana na kadi nyekundu aliyoipata walipokutana na Barcelona katika Mchezo wa
Nusu fainali. Chelsea bado inajivunia wachezaji wake kama Jose Bosingwa , Raul
Mirlaes , Ashley Cole , Mata , Fernendo Torres na Frank Lamaparad t huku
wachwzaji kama Dider Drogba , Salmon Kalou na Studdrige watachangia kuimarisha
makali ya timu hiyo .
Drogba amesema kuwa Chelsea imesubiri kwa miaka mine kufikia
hapa na kuchukua ubingwa, kitu muhimu kwake kwa sasa ni ushindi wa timu yake.
Bayern Munich wana kikosi kizuri leo
wakijivunia hazina ya wachezaji kama Frank
Riberey , Arjen Robben , Mario Gomez , Tomas Mullar , na Bastin Schewnstiger.
Wachezaji wote hawa wataleta burudani kubwa pale Fußball Arena München (Allianz Arena) na chochote kinaweza kutokea
Tunategemea burudani kuu
Tunamsubiri mshindi
Tunawatakia heri -
Tupeni raha
No comments:
Post a Comment