Kinyume cha matarajio ya wengi kwa kuzingatia takwimu za Bahati
nasibu za mshindi, Chelsea FC imelichukua Kombe la mabingwa Ulaya nyumbani kwa
wapinzani wao Bayern Munich. Ushindi ambao umeshuhudiwa na mmiliki wa Chelsea
FC Roman Abramovich.
Chelsea na Bayern Munich kabla ya Mechi
Nakshi iliwekwa uwanjani na mashabiki wa Bayern Munich ikisomeka JIJI LETU, UWANJA WETU, KOMBE LETU
Kwa Abramovich ushindi huu na kile alichokishuhudia
pale Allianz Arena ilikuwa kama ndoto kwani katika miaka yake tisa pale
Stamford Bridge ameshawafukuza makocha nane na kuwasajili wachezaji 66 ambapo
ametumia zaidi ya Paundi Bilioni Moja (£1billion).
Hivyo hakuamini kuwa kikosi hiki cha muda mrefu kilichoanza kuishiwa Nguvu na
Kocha wa Muda wangeweza kuleta kombe Stamford Bridge
Mchezo ulikuwa na mvutano tangu mwanzo mpaka mwisho huku
wenyeji Bayern Munich wakimiliki mpira kwa kiasi kikubwa na kupata Kona nyingi
20 huku Chesea wakipata kona moja iliyozaa goli la kusawazisha.
Goli la kwanza la Bayern Munich lililofungwa Kipindi cha pili dakika ya 83
lilipachikwa kimiani na Thomas Muller Na kufanya uwanja uzizime kwa shangwe,
nderemo na vifijo na kupeleka simanzi kwa mashabiki wa Chelsea. Dakika tano
baadaye kona ya kwanza iliyopigwa na Juan Mata iliunganishwa kwa kichwa na mchezaji Didier Drogba (34)
na kuzaa goli la kusawazisha.
Drogba akishangilia goli alilofunga la kusawazisha
Goli hili kama lilivyokuwa lile la Bayern Munich
lilipokelewa kwa Shangwe kuu na mmashabiki, wachezaji na viongozi wa Chelsea
waliokuwa kwenye benchi la ufundi. Mpaka mpira unakwisha mabao yalikuwa 1 – 1
hivyo kusababisha mpira kuchezwa kwa muda wa nyongeza wa dakika 30 ambao ulishuhudia magoli
yakilala Njaa.
Mikwaju ya penati iliyofuata kwa mujibu wa kanuni ndio
iliyoamua mshindi. Haikuwa rahisi kwa timu yoyote mpaka ulipopigwa mkwaju wa
Mwisho wa penati ndipo mshindi alipatikana. Mkwaju wa mwisho wa penati uliokuwa
ukisubiriwa ambao ulipigwa na Didier Drogba ndio ulioamua matokeo kwani mpaka
ilipopigwa penati ya mwisho ya Bayern Munich mabao yalikuwa 3 -3 huku kila timu
ikiwa imekosa penati moja. Hivyo Mchezo ukamalizika huku Chelsea wakitoka vifua
mbele kwa ushindi wa magoli 4- 3 kwenye
Penati.
Kipa wa Chelsea akiokoa Penati iliyosababishwa na Didier Drogba
wakati wa muda wa nyongeza
Matokeo haya yatabadilisha mtizamo, maamuzi na mikataba
kwa timu, wachezaji, kocha na viongozi wa timu lakini jicho litatupwa zaidi kwa
Roberto Di Mateo aliyeichukua na timu kutoka kwa kocha Andre Villas-Boas wakati ikichechemea na kufanikisha kupeleka
makombe mawili Stamford Bridge. Aidha Didier Drogba ambaye mkataba wake
unaokwisha msimu wa Joto ulikuwa umezungukwa na hisia za kutosainiwa tena
lakini kwa matokeo haya Roman Abramovich ndiye anayejua zaidi.
Goli la kusawazisha la Drogba
Baada ya kupokea kombe hili Drogba alilichukua na
kumpelekea Roman Abramovich akiashiria kumuambia kuwa kazi uliyotutumaa
tumemaliza.
Kazi uliyotutuma Tumemaliza....
Drogba akiondoka uwanjani
Drogba pia alikuwa mtu mweny Furaha sana kwa kuibuka
shujaa na kupingana na kauli ya Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynkes ambaye alipoulizwa kabla ya mechi kuhusu hofu ya kushindwa kutokana na Chelsea
kuwa na washambuliaji mahiri kama Drogba: Jupp Heynkes alijibu na kusema kuwa
Drogba ni muigizaji mahiri tu……
Tumeona leo uigizaji wa Drogba pale alipoipatia timu yake
Goli la Kusawazisha kisha kuipatia ushindi Chelsea pale alipofunga penati ya
Mwisho.
Mpira uliokwamishwa wavuni na mkwaju wa Penati ya Mwisho iliyopigwa na Drogba na kuamua mshindi wa Kombe la Maningwa wa Ulaya
Ushindi huu umesababisha mwanamuziki mashuhuri wa uingereza Jahmaal Noel Fyffe (Chipmunk)Kudiriki kusema
kupitia ujumbe kwenye Mtandao wa Jamii Twitter kwamba “Drogba Ni Chelsea”
Hongera Chelsea
Hongera Di Mateo
Hongera Drogbaaaaa
No comments:
Post a Comment