Huku kukiwa na jitihada za kukaa sawa kwa kikosi cha Liverpool, katika kipindi cha pili, Mchezaji machachari wa Chelsea, Didier Grogba alipiga msumari katika kikosi cha Liverpool na kuifungia timu yake goli la pili katika dakika ya 52.Goli hili likamfanya Drogba kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli katika michezo minne ya fainali ya kombe la FA.
Didier Drogba akifurahia Goli lake
Vijana wa Kenny Dalglish walicharuka katika kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko na kumuingiza Andy Carroll kuchukua nafasi ya Spearing. Kuingia kwa Andy Carroll kulizaa matunda pale ambapo mpira aliochukuwa Andy Carroll huku akimzunguka John Terry ulizaa bao kwa Liverpool ambalo lilianzisha ari na kuongeza kasi ya mchezo. Mabadiliko haya ya kipindi cha pili na bao la lililofungwa na Andy Carrol lilifufua matumaini ya Liverpool kurudisha bao baada ya kufanya mabao kuwa Chelsea 2 - 1 Liverpool.
Wachezaji wa Chelsea walianza kueleka kuchoka ilipofika dakika ya 75 huku mashambulizi ya Liverpool langoni mwa Chelsea yakiongeza kasi. Kenny Daglish aliongeza nguvu katika kikosi chake kwa kumtoa Craig Bellamy na kumuingiza Dirk Kuyt katika kutafuta goli la kusawazisha. Juhudi hizo zilizaa matunda katika dakika ya 82 baada ya mpira wa kichwa uliopigwa na Andy Carroll ulipovuka mstari wa goli na kisha kuokolewa na Petr Cech. Mashabiki wa Liverpool walilipuka kwa furaha wakijua kuwa ni goli lakini muamuzi alitoa uamuzi kuwaonyesha kuwa halikuwa goli. Kitendo kile kililalamikiwa sana na wachezaji wa Liverpool lakini mchezo uliendelea
Mpaka mpira unakwisha, Chelsea imetoka kifua mbele kwa mabao 2 - 1 na hivyo kutangazwa mshindi wa wa Kombe la FA. Hii inakuwa mara ya saba kwa Chelsea kunyakua kombe la FA.
Kombe hili lilipotoka hapa lilielekea Stamford Bridge
Mafanikio haya ya muda mfupi yanaweza kutengeneza njia kwa kocha Roberto Di Matteo kukabidhiwa timu Moja kwa Moja kama kocha Mkuu (Meneja) wa Chelsea
Kocha Roberto Di Matteo
No comments:
Post a Comment