WASHINDI WA KILI MUSIC AWARDS 2012
Tunzo za
Muziki za Kilimanjaro zijulikanazo zaidi kama “Kili Music Awards” Zilifanyika
katika ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Jumamosi ya tarehe 14 Aprili 2012. Safu ya
Wanamuziki waliowania tunzo mwaka huu 2012 ilitawaliwa na majina ya vijana wa
kiume zaidi huku wakike wakionekana
zaidi kwenye vipengele vinavyohusika na jinsia yao.
Kwa
Mujibu wa George Kavishe Meneja wa Bia
ya Kilimanjaro, mchakato wa kuwapata washindi wa tunzo za mwaka huu ulivuka
lengo la idadi ya kura katika njia zote zilizotumika rasmi kwa makusudi hayo
yaani ujumbe mfupi wa simu, vipeperushi, barua pepe na mitandao. Kuvukwa kwa
lengo lililowekwa kunaashiria kukubalika na kupokelewa vema kwa tunzo hizi na Jamii.
Kukamilika kwa shughuli hii ambako hatimaye kulipambwa na nderemo na vifijo
pale Ukumbini Mlimani City Kulishuhudia tunzo hizi zikienda kwa wafuatao:
1) Wimbo Bora Wa Raggae - -Arusha Gold Wa Warriors
From East.
2) Wimbo Bora Wa Dance Hall - Maneno Maneno Wa Queen
Darlin.
3) Wimbo Bora Wa Zouk Rhumba - Dushelele Wa Ali Kiba.
4) 4.Bora Wenye Vionjo Vya Kiasili - Vifuu Utundu Wa
A.T
5) Wimbo Bora Wa Taarabu - Nani Kama Mama Wa Mashauzi
Classic ( Aisha Mashauzi).
6) Wimbo Bora Wa Kiswahili - Dunia Daraja Wa Twanga
Pepeta
7) Wimbo Bora Wa Afro Pop - Hakunaga Wa Suma Lee
8) Wimbo Bora Wa R&B - Number One Fan Wa Ben Paul
9) Wimbo Bora Wa Hip Hop - Mathematics Wa Roma
10) Msanii Bora Anaechipukia Ommy Dimpoz (Nai Nai Singer).
11) Rapa Bora Wa Band -Kalijo Kitokololo
12) Msanii Bora Wa Hip Hop - Roma Mkatoliki
13) Wimbo Bora Wa Kushirikishwa - Nai Nai Wa Ommy
Dimpoz Ft. Ali Kiba
14) Wimbo Bora Wa Afrika Mashariki - Kigeugeu Wa Jaguar
15) Mtumbwizaji Bora Wa Kike - Khadija Kopa
16) Mtunzi Bora Wa Mwaka - Diamond
17) Mtumbwizaji Bora Wa Kiume - Diamond
18) Mtayarishaji Bora Wa Mapigo Ya Muziki - Maneke
19) Video Bora Ya Mwaka - Mawazo Wa Diamond
20) Wimbo Bora Wa Mwaka - Hakunaga Wa Suma Lee
21) Hall Of Fame - Taasisi JKT
22) Hall Of Fame Kwa Mtu Binafsi - King Kikii
23) Hall Of Fame Kwa Mtu Binafsi - Dr. Remmy Ongala
24) Mwimbaji
Bora Wa Kike - Lady Jay Dee
25) Mwimbaji Bora Wa Kiume - Barnaba
Hongera waandaaji wa Kili Music Awards 2012 , Mlitupa
Burudani na kuendelea kutuibulia Vipaji – Kudoz All!

No comments:
Post a Comment