Piermario Morosini(25)
Mchezaji wa kiungo wa timu ya Livorno ya Itali Piermario
Morosini(25) amefariki Dunia baada ya Kuanguka akiwa uwanjani dakika ya 31
wakati timu yake ikipambana na Pescara katika Serie B. Morosini alifariki alipofikishwa
Hospitali katika juhudi za kuokoa maisha yake. Tukio hili linakuja wiki nne tu
baada ya tukio kama hili kumtokea mchezaji wa Bolton kwenye FA Cup Uingereza
Fabrice Muamba ambaye juhudi za kuokoa maisha yake zilifanikiwa. Baada ya
kuanguka Piermario Morosini alijaribu kuinuka na kuanguka tena
Fabrice Muamba (24)
No comments:
Post a Comment