FABRICE MUAMBA ATOKA HOSPITALI
Kwenye Picha hapo juu Muamba anaonekana akiwa
na Madaktari wa hospitali alikolazwa Barts Health NHS Trust Dr Andrew Deaner na Dr Sam Mohiddin
Hatimaye kiungo wa timu ya Bolton ambaye alianguka ghafla uwanjani
tarehe 17 Machi 2012 ameruhusiwa kutoka hospitali leo. Muamba alionekana mwenye
afya na Furaha wakati akitoka hospitali na kuwashukuru wote waliohusika katika
kumhudumia wakati wote alipokuwa hospitali.
Aidha aliwasifu Barts Health NHS Trust kwa moyo wa kujitolea, uweledi na
utaalamu wao katika kipindi chote alichokuwa anapata matibabu. Aidha
aliwashukuru wasamaria wema wote kwa salamu na dua zao za kumtakia heri.
Baada ya kuruhusiwa
kutoka hospitali Muamba atatumia muda huu akiwa na familia yake akiendelea
kupata nafuu
No comments:
Post a Comment