Goli la Fernando Torresi la dakika ya 90 lilipeleka
kilio Nou Camp kwa vijana wa Pep Guardiola katika mchezo wa marudiano kati ya Chelsea na
Barcelona. Huku wakicheza Pungufu kuanzia dakika ya 37 ambapo Mchezaji wa the
Blues John Terry alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Alexis Sanchez, vijana wa Chelsea walipambana
kishujaa mpaka kopenga cha mwisho kilipopulizwa na Mwamuzi wa kimataifa mturuki Cuneyt Cakir. Kadi hii ilitolewa huku Barcelona ikiwa
inaongoza kwa goli 1-0, goli lililofungwa dakika ya 35 na Sergio Besquests
Kuanzia Dakika ya
37 Chelsea waliendelea kucheza wakiwa Pungufu na kukabiliana na wachezaji
machachari na weledi wa kikosi cha Barcelona ambao walikuwa kwenye uwanja wa
Nyumbani, Nou Camp.
Goli lapili kwa
Barcelona liliofungwa na Andrea katika dakika ya 44 liliwafanya Barcelona
kuongoza kwa magoli 2 – 0 na kupeleka matumaini makubwa ya Ushindi kwa
kuzingatia matokeo yao ya awali na Chelsea kule Stamford Bridge.
Nderemo na vifijo
kuchagiza ushindi zaidi kutoka kwa mashabiki wa Barcelona waliohudhuria mechi
hii zilififia kwa Muda katika dakika ya 49 ambapo Ramires aliipatia Chelsea
goli la Kwanza na kufanya matokeo yawe 2-1.
Goli hili
lilifufua matumaini kwa vijana wa Chelsea ambao wamekuwa na kipindi kigumu
katika msimu huu kwenye ligi ya nyumbani hivyo kuwemo kwenye mashindano haya na
hatua waliyoifikia iliwapa matumaini mapya. Matumaini haya yalipandisha mori na
shamrashamra za mashabiki wa Chelsea waliokuwepo uwanjani hapo wakishuhudia
mechi kati ya timu hizi mbili. Hivyo mpaka wanakwenda kwenye Mapumziko Barcelona
walikuwa wanaongoza kwa Magoli 2 – 1
Mashabiki wa Chelsea wakiwachagiza na kushangilia timu yao Uwanjani, Nou Camp
Katika dakika ya
49 Barcelona ilipata Penati ambayo ilipigwa na Lionel Messi, mkwaju ambao uligonga mwamba na
kuikosesha Barcelona kupata goli la tatu. Kukosa Penati hii kunamfanya Messi
kushindwa kupata goli katika Mechi nane mfullulizo walizocheza na Chelsea
Mabadiliko
yaliyofanyika kipindi cha pili kwenye timu ya Chelsea na kumuingiza Fernando Torres
yalipeleka kilio Nou Camp katika dakika ya 90 ambapo Fernando Tores aliifungia
timu yake ya Chelsea goli la kusawazisha. Mpaka Mpira unakwisha matokeo
yalikuwa 2-2 na ukifanya majumuisho ya Mechi zote mbili unapata Jumla ya Magoli
3 kwa Chelsea na 2 kwa Barcelona. Matokeo ya Mechi hii yanaifanya Chelsea iwe
imecheza michezo minne katika uwanja wa nyumbani wa Barcelona Camp Nou bila
kufungwana Barcelona. Katka mechi hizo zote matokeo yalikuwa ni sare. Matokeo haya yalishangiliwa sana na mashabiki
na wachezaji wa Chelsea kwa imitindo mbalimbali
Fernando Torres akishangilia bao lake alilolifunga dakika ya 90
Shangwe kwa wachezaji wa Chelsea baada ya Ushindi
Drogba akishangilia Ushindi wa Chelsea
Branislav Ivanovic akishangilia Ushindi wa Chelsea
Kwa matokeo haya Barcelona inakuwa imetolewa
kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa wa mashindano haya. Aidha John Terry
aliomba msamaha kwa wachezaji wenzake na mashabiki wa Chelsea kutokana na kosa
alilolifanya na kumsababishia Kadi Nyekundu kwenye Pambano lile ambalo
lilihitaji kila aina ya msaada kuihakikisha ushindi timu yake.
Mshindi wa Mchezzo wa leo kati ya Real Madrid
na Bayern Munich ndio utakaoamua timu itakayokutana na Chelsea
No comments:
Post a Comment