Matokeo ya Mechi ya jana ambayo ilizikutanisha timu Mbili real
Madrid na Bayern Munich katika mchezo wa marudiano pale Estadio Santiago
Bernabeu, Madrid yaliitoa Real Madrid nje ya kinyang’anyiro cha ubingwa wa
Kombe la mabingwa baada ya mikwaju ya Penati. Mechi hii ilikuwa ya marudiano
baada ya ile mechi ya kwanza iliyofanyika uwanja wa nyumbani wa Bayern Munich Allianz
Arena, Bayern kumalizika kwa Bayern Munich kuifunga Real Madrid magoli 2-1.
Furaha ya Ushindi - Wachezaji wa Bayern Munich
Goli la dakika ya 6 la mkwaju wa Penati lililofungwa na Chrisian
Ronaldo liliwafanya wenyeji Real Madrid kupata ari zaidi ya ushindi kutokana na
ukweli kwamba goli hilo lilikuwa linafanya matokeo yao ya jumla yawe sare,
hivyo kuifanya iongeze Nguvu ya kutafuta ushindi kuweza kufuzu kuingia katika
fainali ya Ligi hii ya mabingwa.
Pasi ya dakika ya 14 kutoka kwa Mesut Oezel ilimkuta Christian
Ronald akiwa peke yake na hivyo kupiga shuti lililompita mlinda mlango wa Bayern
Munic Manuel Neuer na kuwapa Real Madrid goli la Pili. Bao hili lilifanya Real Madrid iongeze katika mchezo na pia katika jumla ya magoli ya mechi mbili. Nyimbo za furaha na ushangiliaji kutoka kwa mashabiki wa Real Madrid zilizidi kuongezeka kufurahia ushindi
Furaha ya washabiki wa Real Madrid iliingia doa dakika 13 baadaye kutokana na Bayern Munich kupata bao la kwanza. Bao la Arjen Robben wa Bayern
Munich katika dakika ya 27 lilichochea ulinzi na mashambulizi zaidi kutoka kwa Bayern
Munich ambao walikuwa na nia kubwa ya kuona wakiingia fainali ukizingitatia
ukweli kuwa Fainali za kombe la Mabingwa Msimu huu zimepangwa kufanyika Mjini
Munich Ujerumani ambako ni nyumbani kwa timu ya Bayern Munich.Watazamaji
walishuhudia kandanda safi lenye ushindani katika kipindi cha kwanza ambacho likimalizika kwa mabao 2 kwa Real
Madrid na 1 kwa Bayern Munich
Patashika, Piga nikupige, Juhudi na hekaheka za kuwania ushindi kwa wachezaji wa Bayern Munich na wale wa Real Madrid zilitawala katika Mchezo huu
Real Madrid walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda baada ya
kutengeza nafasi nyingi za kufunga na kufanikiwa kupata magoli mawili tu.
Mchezaji wa safu ya mashambulizi Sami Khedira alishindwa kufunga katika dakika
ya tatu baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Angel Di Maria. Lakini mnamo
dakika ya 6 Real Madrid walipata penati baada ya Mpira uliopigwa na Angel Di
Maria kumgonga mkononi David Alaba.
Bayern walipata nafasi mbili ambapo Robben alishindwa kutumia
nafasi iliyotengenezwa na David Alaba na pale ambapo Franck Ribery aliposhindwa
kumalizia mpira uliotokana na mkwaju wa Mario Gomez baada ya kuzuiwa na Mchezaji
wa Real Madrid Khedira
Kipindi cha pili kilishuhudia timu hizi zikimaliza dakika 45
bila kufungana na hivyo kulazimisha muda wa ziada kwa mujibu wa taratibu. Mpaka
kipenga cha mwisho cha muda wa ziada kinapulizwa matokeo yalikuwa Real Madrid 2 Bayern Munich 1 kwa matokeo haya
jumla ya magoli kwa mechi zote mbili ikiwa 3-3. Ili kumpata mshindi, timu hizi
ziliingia katika kipindi cha mikwaju ya penati ambapo Bayern Munich ilifanikiwa
kunasisha wavuni mikwaju 3 dhidi ya mkwaju 1 Ulionasihshwa wavuni na Real
Madrid.
Mlinda mlango makini wa Bayern Munich Manuel Neuer alifanikiwa
kuokoa mikwaju ya Penati ya Ronaldo na Kaka wakati mkwaju wa Sergio Ramos ukipaa
juu ya goli na kufanya mkwaju pekee wa Bastian Schweinsteiger kujaa kimiani. Hii ni
mara ya Pili kwa mashindano makubwa kama haya kushuhudia mfungaji mahiri
Christiano Ronaldo akikosa Penati baada ya kukosa penati kwa mtindo huo mwaka
2008 kwenye fainali dhidi ya Chelsea alipokuwa akiichezea Manchester United
Cristiano Ronaldo baada ya Kukosa Penati
Kwa upande wa Bayern Munic, wachezaji, Mario Gomez, David Alaba na Bastian Scheinsteiger ndio walioizamisha mikwaju ya Penati wavuni.
Bastian akionyesha furaha yake baada ya kufunga mkwaju wa penati na kulizamisha kabisa Jahazi la Real Madrid
Mpira ulimalizika na kuwaacha vijana wa Jupp Heynckes wakitoka uwanjani kifua mbele kwa magoli 3 -1 ya mikwaju ya penati na kufuzu kuingia fainali na Chelsea mapema mwezi ujao.
Kwa matokeo haya Bayern Munich inasonga mbele katika kuwania ubingwa katika fainali itakapopambana na Chelsea katika uwanja wake wa nyumbani Pale Munich, Ujerumani Jumamosi, tarehe 19 Mei 2012
Mchezo huu ulishuhudia kadi saba za njano ambazo ziliwaendea wachezaji wanne wa Bayern Munich na wachezaji watatu wa Real Madrid na hivyo kuathiri timu zao katika fainali.
Bayern Munich italazimika kucheza bila wachezaji wafuatao
itakapopamba na Chelsea kwenye fainali, David Alaba, Holger Badstuber and Luiz
Gustavo. Vile vile Chelsea ambayo itapambana na Bayern Munich itawakosa
wachezaji wake muhimu kama Ramires, John Terry, Branislav Ivanovic na Raul
Meireles kutokana na kupewa kadi katika mchezo wake wa Nusu fainali na
Barcelona.
Kwa mchezo huu wa fainali dhidi ya Chelsea, Bayern Munich itakuwa ni mechi yake ya tisa ya fainali za kombe la mabingwa wakati Chelsea itakuwa ni mechi yake ya pili ya fainali. Katika fainali hizo Bayern Munich imeshinda mara nne wakati Chelsea haijawahi kushinda
No comments:
Post a Comment