Robin Van Persie
Mtikisa Nyavui mahiri wa Arsenal, Robin Van Persie
amechaguliwa kuwa Mchezaji bora wa Mwaka na Muungano wa Waandishi wa Mpira wa
Miguu Uingereza (Football Writers Association). Muungano wa waandishi wa magazeti na wale wa kujitegemea wa Habari za Mpira wa Miguu ulianzishwa mwaka 1947 ukiwahusisha waandishi wa habari za mchezo wa mpira wa miguu Uingereza. Kila mwaka Muungano huu wa wandishi huwa unatoa Tunzo kwa Mchezaji bora wa mwaka ambaye ametoa mchango mkuwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Tunzo hii ni kati ya tunzo kuu mbili zinazoheshimika sana katika Soka la Uingereza; tunzo nyingine ni ile inayotolewa na Muungano wa wachezaji wa Kulipwa wa Mpira wa miguu (Professional Footballers Association) yaani Tunzo ya Mchezaji bora wa Mwaka ya PFA. Tunzo hii imeanza kutolewa rasmi kwenye msimu wa 1973/4
Ushindi wa kishindo wa Van Persie katika tunzo iliyotolewa na FWA umetokana na kura
takribani 400 za waandishi wa habari matokeo ambayo yamemuacha nyuma Mtikisa
nyavu wa Manchester United Wayne Rooney. Aliyefuata katika kura hizo ni mchezaji
wa Manchester United Paul Scholes huku nafasi ya nne ikikamatwa na Mchezaji wa
Fulham Clint Dempsey.
Tunzo hizo mbili kwa mpigo zinamfanya Van Persie
kuwa mchezaji wa 16 kuchukua tunzo mbili kwa wakati mmoja. Mchezaji wa mwisho
kupata tunzo hizo kwa mpigo alikuwa Wayne Rooney mwaka 2010
Van Persie amefunga Jumla ya Magoli 34 katika
mashindano yote yakiwamo 27 katika ligi
Video Clip hapo chini inamuonesha Robin Van Persie akifunga goli katika Mechi dhidi ya Everton
No comments:
Post a Comment