Mazungumzo marefu kati ya Kocha wa Barcelona, Pep Guardiola leo Jumanne 27 Aprili 2012 na Raisi wa timu
Sandro Rosell yaliishia katika tamko
rasmi la Pep kutosaini mkataba mwingine na Bracelona. Hatua hi inakuja baada ya
kushuhudia Barcelona ikiondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ushindi
katika kombe la mabingwa dhidi ya Chelsea.
Kabla ya kutangaza uamuzi huu, Guadiola aliongea na
wachezaj wake wakati wa Mazoezi asubuhi ya leo kuhusu uamuzi wake wa kutosaini
mkataba mwingine wa kukinoa kikosi cha Barcelona. Guardiola anaondoka Nou Camp
baada ya miaka minne ya mafanikio kama Kocha wa Barcelona. Guardiola alanza
kukifundisha kikosi cha kwanza cha Barcelona akitokea Barca B mwaka 2008; hatua
ilyomfanya awe kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Barca.
Guardiola aliiongoza Barcelona kuchukua ushindi marambili
kwenye ligi ya mabingwa, makombe matatu La liga, ushindi mara moja kwenye Copa
del rey, makombe matatu kwenye supercopas, Makombe mawili ya UEFA super Cups na
makombe mawili ya Fifa Club world Cups. Anaondoka Nou Camp akiwa amefanikisha
ushindi wa makombe 13 Barcelona katika miaka minne.
Pep Guardiola akiwa ameshika kombe la
Mabingwa Mei 2011 baada ya kuifunga Manchester United, Wembley Stadium
Hata hivyo kutolewa na Chelsea kwenye kinyang’anyiro cha
ubingwa wa kombe la mabingwa kulikuja siku tatu baada ya kufungwa na wapinzani
wao wakubwa Real Madrid kwenye uwanja wa nyumbani na kupeperusha matumaini ya
kunyakua ubingwa wa ligi ya nyumban (Primera Division Crown). Kipigo hiki cha
Real Madrid kiliweka tofauti ya pointi saba baina ya timu hizi mbili huku
wakiwa wamebakiwa na michezo minne mkononi
Guardiola amekishikilia kikosi cha Barcelona ka kusimamia
maendelo ya timu na wachezaji wake akishuhudia Loinel Messi akiwa mchezaji bora
wa mwaka mara tatu na kuimarisha kiwango cha wachezaji kama Xavi na Iniesta.
Mafanikio na majina ya wachezaji haya yamekuwa yakibeba usanifu wake.
Raisi wa Barcelona Sandro Rosell
Raisi, Rosell ametoa shukrani zake za dhati kwa Pep
Guardiola kwa Furaha ambayo ameipatia Barcelona kipindi chote cha utumishi
wake.
Siku zote Guardiola amekuwa akisisitiza kufanya chochote ambacho ni bora
kwa Barcelona hivyo wakati wa mazungumzo marefu na Raisi wa Klabu, Guardiola aliendelea kusisitiza msimamo wake wa kutoendelea
kuifundisha klabu yake akiamini hicho ndicho kitu bora kwa klabu.
Kwa heri Guardiola!
No comments:
Post a Comment