F
|
abrice Muamba ameongea kwa mara ya kwanza kuhusu tukio la kutisha
alipoanguka kiwanjani dakika ya 41 wakati timu yake ya Bolton ikicheza na
Tottenham tarehe 17 Machi 2012. Kitaalamu kuanguka na kupoteza fahamu kwa
Muamba kulitafsiriwa kama Kifo cha dakika 78. Iliwachukua madaktari Mistuo ya
Moyo mitatu (defibrillator shocks) kuufanya moyo wa Muamba uanze kufanya kazi
tena. Alifanyiwa mishtuko hiyo mara mbili kiwanjani na mmoja akiwa kwenye gari
la wagonjwa kueleka Hospitali.
“Nilikuwa
nakimbia, nikasikia kizunguzungu, nikawa sioni ...kisha nikajihisi nikianguka”
“...Nilikuwa nakimbia kuifuata pasi
iliyopigwa na Martin Petrov kwa kiungo chetu cha kushoto na nilipokuwa narudi
kati nikahisi kizunguzungu kidogo.. hakikuwa kizunguzungu cha kawaida, nilikuwa
kama nakimbia kwenye mwili wa mtu mwingine, nikaendelea kukimbia, nikahisi tena
kizunguzungu macho yakapoteza nuru- sikuwa na maumivu yoyote wala mguso wowote kifuani.
Nikaanza kuona vitu viwili viwili. Nilihisi kama ndoto. Hakukuwa na yoyote
karibu yangu nilipohisi kuanguka.
Kitu cha mwisho ninachokumbuka ni sauti
ya Dedryck Boyata (Mchezaji wetu katika safu ya Ulinzi) akiniambia kwa sauti
nirudi nyuma na kusaidia safu ya ulinzi. Nilijihisi nikianguka na kuhisi
vishindo viwili kichwa changu kilipogonga ardhini. Giza, hakukuwa na kitu,
nilikuwa mfu”.
Wachezaji wakiwa na Simanzi baada ya Muamba Kuanguka na kupoteza fahamu uwanjani
Muamba anategemea kuwepo uwanjani tarehe 2 Mei kushuhudia mpambano wakati
timu yake ya Bolton itakapopambana na Tottenham ikiwa ni marudio ya mechi
iliyoahirishwa siku alipoanguka uwanjani.
Muamba anakumbuka kuwa kabla ya Mechi ile aliomba ulinzi wa Mungu. Alisema
Mungu alikuwa pamoja naye kwani kilichotokea ni zaidi ya muujiza.
“Siku ya Mechi nilisali na Baba yangu
kumuomba mungu anilinde na Mungu hakuniangusha. Ninatembea kwa ushuhuda wa nguvu
za Maombi. Kwa dakika 78 nilikuwa mfu na kama ningeishi ningepata madhara
makubwa kwenye ubongo. Lakini mimi ni mzima sana nimekaa na ninaongea. Mungu
alikuwa ananiangalia na kunilinda”
Muamba amewekea Kifaa kwenye kifua cha kuzuia (efibrillator) shambulio kama hilo endapo litatokea. Kwa sasa Muamba anaangaliwa kwa ukaribu na timu imesema wazi kuwa endapo
Muamba atapenda kuhudhuria mechi ya Bolton itategemea zaidi hali yake ya kiafya
No comments:
Post a Comment