Kwa Nini El-Clasico?
El
Clásico ambayo hujulikana pia kama El Derbi Espanol ni jina linolotumiwa wanapokutana mafahari wawili
wa Soka wa Hispania yaani Real Madrid
na FC Barelona. Katika ligi, timu
hizi hukutana mara mbili kwa mwaka au hukutana tena endapo timu hizi zitakutana
katika mashindano mengine kama UEFA. Timu hizi ndizo zinavuta mashabiki,
wafuatiliaji na watazamaji wengi zaidi duniani zinapokutana ukiacha mashindano
ya UEFA. Ushindani huu unaovuta hisia za watazamaji na wafuatiliaji wengi
unatokana mafanikio ya timu hizi
katika Soka, utajiri, na ukubwa wa miji zinatokea timu
hizi yaani Madrid na Barelona. Real Madrid haijawahi kushuka
daraja tangu ilipoanzishwa.
Wakati mwingine ushindani huu wa soka baina ya
timu hizi mbili umehusishwa mpaka kwenye nyanja
za siasa za Hispania ambapo Real Madrid inahusishwa na hama cha Spanish
Nationalism wakati Barcelona inahusishwa na Calatan Nationalism. Ushindani wa
timu hizi ndioo unaoaminika kuwa mkubwa zaidi katika ulimwenu wa soka Duniani.
Na hii ndio inavuta hisia za watu wengi zaidi ulimwenguni
CHRISTIANO
RONALDO AIZAMISHA BARCELONA NYUMBANI NOU CAMP
Goli
la dakika ya 73 kipindi cha pili la Christiano Ronaldo (27) liliihakikishia
Real Madrid Ushindi ambao uliipadisha Real Madrid kwa tofauti ya Pointi saba
(7) Mbele ya Washindani wao wakubwa Barcelona. Ushindi huu ulipatikana nyumbani
kwa timu hiyo bora duniani Barcelona pale Nou Camp Jumamosi ya Tarehe 22 Aprili
2012.
Timu
zote mbili zilikuwa zimetoka katika mechi za UEFA ambapo zote zilipoteza katika
round hiyo; Mechi hizo zilishuhudia Barcelona ikifungwa Bao Moja na Chelsea
Jumatano tarehe 18 Aprili 2012 pale Stamford Bridge na Real Madrid ilifungwa 2 –
1 na Bayern Munich Jumanne tarehe 17 April 2012, Muuaji wa Real Madrid akiwa
Mario Gomez ambaye aliupeleka mpira Kimiani na kupata goli la Pili katika
dakika ya 90
Kwa ushindi huo, Real Madrid imesafisha njia kueleka kwenye Ubingwa wa Ligi ya Hispania
No comments:
Post a Comment