Kupatikana kwa jina
la mrithi wa Guardiola, Tito Vilanova (42) mara tu baada ya kutangazwa kuondoka
kwa Guardiola kwenye mkutano wa waandidhi wa habari kulishangaza wengi. Awali
kulipokuwa na tetesi za Guardiola kutotia saini mkataba mwingine, majina ya
makocha maarufu yalikuwa yakitajwa tajwa na wadau mbalimbali; majina kama Ernesto Valverde, Laurent Blanc na Marcelo Bielsa
Kocha Mteule Tito Vilanova (42)
Akitangaza jina la kocha mpya,
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Andoni Zubizarreta alisema kuwa ni utaratibu
wa Barcelona kuwa siku zote wanaposaka wachezaji huwa wanaanza kuangalia ndani
ya timu yao kwanza kisha wanatafuta nje. Hivyo aliyekuwepo na kuweza kumudu
nafasi hiyo ni Tito Vilanova.
Aliendelea kusema kuwa Tito
Vilanova anawakilisha aina yao ya mchezo na mawazo yao na kwamba hakuna kocha mwingine
kutoka nje ya timu ambaye angeweza kufanya hivyo. Ni wazi kuwa Tito yuko
tofauti na Guardiola lakini atafanya kazi katika mtazamo ule ule.
Tito Vilanova aliwahi kuwa mchezaji wa kiungo wa Barcelona ambapo alicheza
michezo 26 ya ya ligi ya hispania (La Liga). Alichaguliwa kuwa msaidizi wa
Kocha wa Barcelona B mwaka 2007 chini ya Guardiola. Baada ya kuonyesha
mafanikio katika kikosi hicho wote wawili Tito na Guardiola walipandishwa
daraja na kuanza kukifundisha kikosi cha kwanza cha Barcelona mwaka 2008.
TITO VILANOVA NI NANI?
· Alizaliwa
tarehe 17 Septemba, 1969 Bellcaire
d'Emporda Girona, mji unaopatikana Gerona, Cataluna, huko Hispania
· Mwaka 1988 akiwa na Pep Guardiola
alijiunga na Barcelona B ambapo alicheza kwa miaka miwili
·
Mwaka 1990 alicheza:lower-league Figueres.
·
Mwaka 1992:alihamia Primera Division
Celta Vigo lakini hakupata nafasi katika kikosi cha kwanza
· Mwaka 1995 aliondoka Celta na kuchezea ligi mbali mbali kati ya mwaka 1995 mpaka 2002 akiwa na timu kama:
o
Club Deportivo Badajoz
o
Real Club Deportivo Mallorca,
o
Unió Esportiva Lleida
o
Elche Club de Fútbol
· Mwaka 2002 alistaafu kucheza soka akiwa
katika timu ya Unión
Deportiva Atlético Gramenet Milán (Gramenet)
· Baada ya kustaafu soka aliendelea kuwepo katika fani ya
soka mpaka alipofikia kuwa Mkurugenzi wa ufundi Tarrasa, timu ambayo uwanja
waake wa nyumbani Estadi Olímpic de Terrassa, una uwezo wa kuchukua
watazamaji 11.500. Aliondoka Terrassa akiiacha timu hii katika nafasi ya 6 katika
ligi ya Segunda Division B
· Mwaka 2007 alijiunga na Barcelona B kama
msaidizi wa Kocha Pep Guardiola ambapo waliisadia timu kupanda daraja kwenda Segunda Division B.
·
Mwaka 2008 Tito alipandishwa daraja kuwa
msaidizi wa kocha Pep Guardiola katika Kikosi cha Kwanza cha Barcelona. Makocha
hawa wawili walileta mafanikio makubwa katika kikosi hiki cha kwanza kwa
ushindi wa vikombe mbalimbali kwenye ligi ya ndani, ligi ya Ulaya na klabu
bingwa ya dunia
·
Tarehe 27 Aprili 2012 Tito Vilanova anateuliwa kuwa
Kocha wa kikosi cha kwanza cha Barcelona kuanzia msimu ujao kufuatia kuondoka
kwa Kocha Mkuu Pep Giuardiola ambaye alisema kuwa hakuwa na nguvu tena za
kuongoza timu na kupata zaidi kutoka kwa wachezaji kwenye kila mchezo. Pep
alisema anahitaji kupumzika baada ya mchango wake wa miaka minne katika timu.
Baada ya kutangazwa jina la Tito Vilanova kama kocha mkuu wa wa Barcelona kwa
kikosi cha kwanza, Pep Guardiola alionyesha kuridhishwa na uteuzi huo. Pep
alisema kuwa klabu imefanya uamuzi bora kwa maendeleo ya tmu kwa vile anaamini
kuwa Tito Vivanola ana uwezo mkubwa na wachezaji wanamjua vema. Anajua kuwa
Tito atafanya mabadiliko machache na kuwapa wachezaji na klabu kile ambacho
yeye asingeweza kuwapa kwa wakati huu.
Messi akikumbatiana na Pep Guardiola baada ya kuwaarifu juu ya uamuzi wake mazoezini
Pep Guardiola akiaga baada ya mkutano wa waandishi wa habari
Tito Vilanova - Pamoja!
No comments:
Post a Comment