WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Saturday, May 9, 2015

TIBA YA MOYO BILA UPASUAJI MUHIMBILI - MAENDELEO YA KITEKNOLOJIA

"CATH LAB" Mtambo unaotumika Kufanya Uchunguzi, Kuzibua Mishipa inayopeleka damu kwenye Moyo na kuziba matundu ya Moyo bila Kufanya Upasuaji Ulioko Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Idara ya Tiba na Upasuaji Moyo.

Katika hatua nyingine ya kimaendeleo katiba tiba, Kitengo cha Tiba ya Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, imefanikiwa kufanya Tiba ya Moyo kwa kuziba Matundu ya Kwenye Moyo Bila Kufanya Upasuaji wa Kifua. Hii inatokana na Maendeleo ya Kiteknolojia na matumizi ya Mtambo wa kufanya Uchunguzi, Kuzibua Mishipa ya Damu na Kuziba Matundu ya kwenye Moyo.

Tiba hii imefanyila lwa Kushirikiana na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre ya Riyadh Saudi Arabia.

Hii ni hatua nyingine kubwa katika nyanja ya Tiba na Afya baada ya Kushuhudia ushirikiano kama huu na Hospitali mbalimbali za kimataifa kwa kutumia mifumo ya Habari kama Video Conference ambapo madaktari waliweza kufanya upasuaji nchini kwa kushirikiana na Madaktari bingwa wenzao walioko nje ya Nchi.

Baada ya Uzibaji huu wa Moyo bila upasuaji, Kaimu Murugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dr. Hussein Kidanto, amesema zaidi ya wagonjwa  ishirini (20) wanatarajiwa kupata Tiba ya Moyo kwa Utatatibu huu.

No comments:

Post a Comment