WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Sunday, September 29, 2013

MISS PHILIPPINES ATUNUKIWA TAJI LA MISS WORLD 2013

 Megan Young ambaye ni Miss Philippines ametunukiwa taji la kuwa Miss World mwaka 2013 katika fainali iliyofanyika Indonesia, Nusa Dua Kwenye Kisiwa cha Bali  chini ya ulinzi mkali kutokana na upinzani mkubwa kutoka kwa Waisilamu wenye msimamo mkali wanaopinga mashindano hayo.

Megan Young, Miss Philippines baada ya Kuvikwa Taji la Miss World 2013, siku ya Jumamosi Septemba 28, 2013
Miss world 2013, Megan Young akipongezwa na Miss World 2012,  Yu Wenxia aliyemaliza Muda wake

Miss World 2013 Megan Young akiwashukuru watazamaji baada ya kutunukiwa Taji huku akiwa na Mshindi wa Pili na wa Tatu wa Shindano hilo Miss France na Miss Ghana

Miss World akiwa na washiriki wengine mara baada ya Kutangazwa Mshindi wa Shindano hilo la Dunia, 2013
Miss Philippines akipita kwa Mwendo wa kunyata "Cat Walk" kabla ya kutangazwa mshindi wakati kinyang'anyiro kikiendelea
Ulinzi Mkali nje ya jengo yalimofanyika Mashindano ya Miss World 2013

Askari wakifanya doria kuzunguka Jengo yalimofanyika Mashindano ya Miss World 2013
Waislamu wenye msimamo Kali wakipinga kufanyika kwa Mashindano hayo wakiyaona kuwa ni haramu

Waislamu wenye msimamo mkali wakipinga kufanyika kwa mashindano hayo 

No comments:

Post a Comment