WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Tuesday, November 13, 2012

MZUNGUKO WA LIGI KUU TANZANIA BARA WAKAMILIKA



Matokeo ya Mechi ya Jumapili tarehe 12 November 2012 baina ya Yanga na Coastal Union pale Mkwakwani yalim-bainisha kiongozi wa ligi hiyo katika mzunguko wa kwanza huku mechi chache zikibaki kukamilisha mzunguko huo

Tumeshuhudia mengi katika Mzunguko huu wa Kwanza; harakati, mikakati na juhudi mbalimbali kujiimarisha katika msimamo wa Ligi. Harakati hizo zimeshuhudia Furaha na Amani hali kadhalika huzuni na ghadhabukwa upande mwingine katika vilabu vya soka vinavyoshiriki ligi hii. Lakini kama wasemavyo wengi, Soka ni mchezo wa Makosa! Makosa yako wewe huwa nafasi kwa mpinzani wako endapo atayatumia Vema kama tulivyoona kwenye michezo mbalimbali katika mzunguko huu.

Kuna mengi tumeyaona yanayohusisha Vilabu, Kamati ya Ligi, Wadhamini, Wanachama, viongozi na wadau wote wa soka. Basi kipindi hiki cha mapumziko kitakuwa kipindi muafaka kutathmini yote yaliyojitokeza ili tuweze kuifanya ligi na mashindano haya kuwa Bora zaidi.

Msimamo mpaka mwisho wa ligi hii ulikuwa hivi:

Nafasi
Timu
MP
W
D
L
GF
GA
+/-
Pts
1
Young Africans
13
9
2
2
25
10
15
29
2
Azam
13
7
3
3
17
11
6
24
3
Simba SC
13
6
5
2
20
11
9
23
4
Mtibwa Sugar
13
6
4
3
18
12
6
22
5
Coastal Union
13
6
4
3
16
14
2
22
6
Kagera Sugar
13
5
6
2
15
10
5
21
7
Ruvu Shooting
12
5
2
5
17
17
0
17
8
JKT Ruvu
13
4
3
6
13
20
-7
15
9
Tanzania Prisons
11
3
5
3
8
9
-1
14
10
JKT Oljoro
13
3
5
5
13
16
-3
14
11
Mgambo JKT
12
4
2
6
9
13
-4
14
12
Toto African
13
2
6
5
10
15
-5
12
13
African Lyon
13
2
3
8
9
20
-11
9
14
Polisi Morogoro
13
0
4
9
4
16
-12
4

 

Kipindi hiki pia kitatoa muda wa mapumziko kwa wachezaji ambao katika mzunguko mzima wamekuwa wakichua njumu za viatu vyao kwenye nyasi za viwanja katika juhudi ya kujiweka sawa. Ni katika mapumziko haya ambapo kutakuwa na mwezi mmoja kuanzia tarehe 15 Novemba 2012 ambao utatoa nafasi ya Usajili, uhamisho na taratibu zote za mikataba ya wachezaji mpaka hapo tarehe 15 Desemba 2012.

Wapenzi na wadau wa soka wanasubiri kwa hamu mwamzo wa mzunguko wa pili wa Ligi kuu itakayoanza tarehe 19 Januari 2012 wakitegemea kuona soka bora zaidi, ushindani na usimamizi bora wa Ligi kuu. Furaha ya Wapenzi wa soka ni kupata mshindi ambaye atatokana na umahiri na ueledi wake katika soka. Hivyo mwisho wa ligi hii tarehe 20 Aprili 2012 unategemea kutoa taswira hiyo njema ya soka letu la Tanzania

 

No comments:

Post a Comment