WEZESHA WANAWAKE

WEZESHA WANAWAKE

Monday, January 28, 2013

MSANII WA FILAMU LULU AACHIWA KWA DHAMANA

Mahakama Kuu ya Tanzania imekubali dhamana ya Msanii Elizabeth Michael au maarufu kama  Lulu iwapo atatimiza masharti yote ya dhamana hiyo.
Elizabeth Michael "Lulu"
 
Lulu alishitakiwa na kutuhumiwa kuhusu Kifo cha Msanii mwingine wa Filamu Nchini Marehemu Steven Kanumba. Toka wakati huo, Lulu amekuwa Chini ya Ulinzi mahabusu kutokana na kesi hiyo inayomkabili. Dhamani hii kwa mara ya kwanza itamuwezesha Lulu kuishi nje ya Mahabusu tangu mwezi wa Aprili 2012 alipowekwa chini ya Ulinzi Mahabusu.
 
Lulu akiwa Mahakama kuu ya Tanzania Leo
 
Furaha ya Lulu haikuweza kufichika akiwa mahakamani Leo
Maisha ya Lulu akiwa chini ya Ulinzi wakati kesi ikiwa Mbichi
 
Shauri la Lulu wakati likiwa katika Mahakama ya Kisutu kabla ya Kupelekwa Mahakama Kuu
 Lulu akirudi mahabusu wakati shauri lake likiwa katika hatua za awali
Lulu kabla ya kukutwa na misukosuko ya Kesi inayo mkabili
 
Kwa amri hii ya mahakama Kuu ya Tanzania iliyoruhusu dhamana ya Elizabeth Michael kwa Masharti matano, Lulu hatimaye atarudi uraiani kujumuika na familia, Marafiki, ndugu, Jamaa na mashabiki wake baada ya kuwa nao mbali kwa takribani miezi kumi

No comments:

Post a Comment