Raisi Mteule Francois Hollande (57)
Zile mbio za kuwania Kiti cha Uraisi wa Ufaransa zimefikia
ukingoni baada ya Nicolas Sarkozy kukubali
kushindwa na mpinzani wake bwana Francois Hollande katika Uchaguzi wa kumtafuta
Raisi wa Ufaransa katika awamu ya Pili kwa tofauti ya 3.4%. Nicolas Sarkozy ambaye ni Raisi wa 23 wa Ufaransa aliingia madarakani tarehe 16 Mei 2007 na antegemea kuachia madaraka tarehe 17 Mei 2012
Francois Hollande anatoka
katika Mrengo wa kushoto wa siasa za Ufaransa katika chama cha Socialist Party
(PS). Alipoanza harakati za kuwania nafasi hii ya juu katika nchi ya Ufaransa
kabla ya kashfa ya ngono dhidi Dominique Strauss-Kahn ambaye ndio alionekana
kuwa mpinzani makini wa Nicolas Sarkozy, Hollande alionekana kama akipoteza
wakati wake.
Raisi Mteule Francois Hollande
Ushindi wa Raisi Mteule Francois
Hollande (57) unabadilisha muelekeo wa siasa za Ufaransa kutoka Mrengo wa kulia
kwenda kushoto baada ya takribani miaka 20. Ushindi huu unapatikana wakati
Ufaransa ikiwa katika jitihada za kupambana na mtikisiko wa Kiuchumi ambao
umeiathiri Ufaransa pamoja na nchi nyingine za Ulaya.
Wafuasi wa Raisi Mteule Francois Hollande wakifurahia Ushindi
Kundi la Vijana kutoka katika Chama chaSocialist Party(PS) wakigonganisha Glasi za Mvinyo kufurahia Ushindi
Raisi anayeondoka
madarakani Nicolas Sarkozy, anatoka madarakani baada ya uongozi wa nchi hiyo
katika kipindi kimoja na kumfaya kuwa Raisi wa 11 kushindwa katika kinyang’anyiro
cha Uraisi katika nchi za Ulaya toka Mtikisiko wa Uchumi ulipoanza mwaka 2008.
Pamoja na sababu zingine, wataalamu na wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanaona
kuwa Mtikisiko wa kiuchumi umechangia katika kushindwa katika chaguzi
mbalimbali kwa Maraisi walioko katika Jumuiya ya Ulaya.
Kwaheri Raisi Nicolas Sarkozy
Baada ya Kukuabli
matokeo yaliyompa Ushindi Raisi Mteule Francois Hollande, Raisi Nicolas Sarkozy
amewashukuru wafuasi wake na wote waliomsaidia katika kinyang’anyiro cha kuwania
Uraisi wa Ufaransa katika awamu ya Pili. Alisema kuwa alijaribu kwa kadri ya
uwezo wake kushinda katika kinyang’anyiro hiki lakini ikashindikana. Anajua
kuwa wananchi walikuwa na hasira na jinsi ambavyo amekuwa akishughulikia suala
la Uchumi wa Ufaransa lakini amekubali kuwajibika kwa matokeo ya Uchaguzi huo.
Aidha Nicolas Sarkozy
baada ya kukubali matokeo ya Uchaguzi alimtakia kila la kheri Raisi Mteule Francois
Hollande.
Raisi Mteule Francois
Hollande aliwashukuru wapigakura wote huku akiahidi kuwa Raisi wa wote, yaani
wa waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura. Alisisitiza kuwa yeye ni
mtu wa Kawaida na atafanya kazi kuinua uchumi uliotetereka na kushughulikia
ahadi yake ya kusimamia Haki na masuala ya Vijana.Raisi Mteule Francois Sarkozy attanza Kazi rasmi tarehe 17 Mei 2012
Kufuatia Ushindi huo
Raisi wa Marekani, Barack Obama, ambaye naye yuko katika harakati za kuwania
ofisi hiyo ya Uraisi wa Marekani kwa awamu nyingine, alimpigia simu Raisi
mteule Francois Hollande na kumpongeza kwa Ushindi alioupata
No comments:
Post a Comment